55. Ni wajibu kuwachukia makafiri na kuwachukulia maadui

Kisha baada ya kujua uwajibu wa kuwakufurisha washirikina na makafiri yeyote awaye na kwamba hii ni ´Aqiydah ambayo Uislamu wala dini haisihi na kusimama isipokuwa kwayo na watu wote mbele ya muislamu hawawi sawa, bali lazima atofautishe baina ya haki na batili, muumini na kafiri na mkanamungu. Anatakiwa kutofautisha baina yao kama jinsi Allaah alivyowatofautisha katika hukumu.

Juu la suala la kuwakufurisha makafiri kunazuka hukumu mbalimbali. Tutataja zile zitazokuwa sahali:

1- Ni wajibu kuwachukia makafiri, kuwafanya maadui na kutofanya nao urafiki. Haijalishi kitu hata kama atakuwa ni ndugu wa karibu kabisa na muislamu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ

”Enyi mlioamini! Msimfanye adui Wangu na adui wenu marafiki wandani mkiwapelekea [siri za mikakati] kwa mapenzi na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni. Wanamtoa kwa kumfukuza Mtume pamoja na nyinyi kwa vile tu mmemuamini Allaah, Mola wenu; ikiwa mmetoka kwa ajili ya Jihaad katika njia Yangu na kutafuta radhi Zangu. Mnawapa siri kwa mapenzi na hali Mimi najua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Na yeyote yule atakayefanya hivyo katika nyinyi, basi hakika amepotea njia ya sawa.” (al-Mumtahinah 60:01)

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

”Hakika mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, pale walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali kabisa nanyi na yale yote mnayoyaabudu badala ya Allaah. Tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya milele mpaka mumuamini Allaah pekee.” (al-Mumtahinah 60:04)

Vilevile amesema (Ta´ala):

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ

”Hutowapata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho  kwamba wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, ijapo wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao – hao Amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa roho kutoka Kwake.” (al-Mujaadilah 58:22)

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا

”Basi yule atakayemkanusha Twaaghuut [waungu wa uongo] na akamwamini Allaah, basi kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.”(al-Baqarah 02:256)

Hii inafahamisha kwamba imani ya kumuamini Allaah na kuamini Twaaghuut ni mambo mawili yasiyoweza kukusanyika. Bali ni lazima kwa mtu kwanza akufuru twaaghuut kisha ndio amuamini Allaah (´Azza wa Jalla). Vilevile ni wajibu kukufuru twaaghuut na kuwafanya makafiri kuwa maadui na kuwachukia hata ikiwa ni watu wa karibu sana na muislamu. Haijalishi kitu hata atakuwa ni baba yake, mama yake, mtoto wake, kaka yake, kutoka katika kabila lake na jamaa zake. Anatakiwa kumchukia na kujiweka mbali naye. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ

”Haiwi kwa Allaah awapotoze watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie ya kujikinga nayo.” (at-Tawbah 09:115)

Pindi Allaah alipoteremsha Aayah hizi wakasikitika watu katika waislamu ambao walikuwa wakiwaombea msamaha baba zao washirikina ambao wameshakufa na wakaogopa Aayah hii. Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ

”Haiwi kwa Allaah awapotoze watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie ya kujikinga nayo.”

Hawatochukuliwa hatua juu ya yale yaliyopitika kabla ya kuteremshwa Aayah na kabla ya waislamu kujua uharamu wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 26/09/2018