55. Ngazi nne za Qadar


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Inatakiwa kuamini Qadar, nzuri yake na shari yake, tamu yake na chungu yake. Yote hayo ameyakadiria Allaah, Mola wetu. Makadirio ya vitu yako mikononi Mwake. Yanatokamana na mipango Yake.

MAELEZO

Kuamini makadirio na mipango ni moja katika nguzo za imani. Yanajulishwa na Hadiyth ya Jibriyl pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Imani ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar, nzuri yake na shari yake.”[1]

Makadirio ni yale ambayo Allaah ameyakadiria na kuyapanga na akayaandika katika Ubao uliohifadhiwa.

Daraja za kuamini Qadar ni nne:

1 – Ujuzi. Allaah alikijua kila kitu kwa ujuzi Wake wa milele na wa daima.

2 – Uandishi. Akakiandika kila kitachotokea katika Ubao uliohifadhiwa mpaka siku ya Qiyaamah.

3 – Utashi. Anapotaka kitu kitokee basi hufanya hivo. Hakukuwi katika ufalme Wake kile akichokitaka.

4 – Uumbaji. Allaah ameumba kila kitu. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ

”Allaah ni muumbaji wa kila kitu.”[2]

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar.”[3]

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ

”Allaah ni muumbaji wa kila kitu.”[4]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameumba kila kitu kilichokuweko na kitachokuweko.

[1] Muslim (8).

[2] 39:62

[3] 54:49

[4] 39:62

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 03/08/2021