1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msichukiane. Msishindane. Msihusudiane. Msipeane migongo. Kuweni waja wa Allaah ndugu.”

2 – Haijuzu kati ya waislamu kuchukiana, kushindana, kuhusudiana wala kupeana migongo. Ni lazima kwao kuwa ndugu kama alivoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati mmoja wao anapopatwa na maumivu basi mwingine anahisi maumivu yake. Wakati mmoja wao anapofurahi basi mwingine anafurahi kwa furaha yake. Hafanyi udanganyifu. Anaona kuwa nafsi zimejisalimisha kwa Allaah (´Azza wa Jall). Ni mwenye kuridhia makadirio yote ya Allaah. Haijuzu kwa waislamu kukatana kwa kupatikana kosa kutoka kwa mmoja wao. Bali ni wajibu kwao kuligeuza katika mkabala mzuri na kuoneana huruma na kuacha kususana.

3 – Mtu hatakiwi kuwa kama ambaye hakusoma na mjinga kwa kuchafua mapenzi kwa ndugu zake kwa sababu ya mambo yanayopelekea katika kukatana ambako amekataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali anapaswa kuyafumbia macho makosa na kuacha kujadili makosa yaliyofanywa. Hili khaswa katika mambo ambayo kuna uwezekano yakawa ya kweli au ya batili.

4 – Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan amesema:

“Nimemsikia Abu ´Ammaar al-Husayn bin Hurayth akisema: “Kuna bwana mmoja aliulizwa kama yeye anazo kasoro. Bwana yule akajibu kwamba hana. Akaulizwa kama kuna yeyote ambaye anazitafuta. Akajibu kuwa yupo. Ndipo akaambiwa: “Basi ni wingi ulioje wa kasoro zako!”

5 – Yapo mambo matatu yanayopelekea kususana kati ya waislamu; kosa la ndugu, jambo ambalo haliepukwi, kashfa na uchoshi wa mbeya uliofungamana na kitu katika michango hii miwili. Uchovu unapelekea katika mahusiano yaliyokatwa. Mtu anayechosha hawi na rafiki.

6 – Haijuzu kwa muislamu kumsusa ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu. Anayefanya hivo anakuwa ametumbukia katika makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).  Mbora wao ni yule mwenye kuanza kutoa salamu. Wa mwanzo wao kutoa salamu ndiye atakuwa wa mwanzo wao kuingia Peponi. Mwenye kumsusa ndugu yake mwaka mzima ni kama kumuua. Anayekufa hali ya kuwa amemsusa ndugu yake anaingia Motoni ikiwa Allaah hatomsamehe na kumrehemu. Haifai kwa waislamu kukatana zaidi ya siku tatu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 204-207
  • Imechapishwa: 23/08/2021