55. Je, madhiy yanaharibu swawm?

Swali 55: Kuna mtu amecheza na mke wake mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga ambapo akatokwa na madhiy. Je, swawm yake ni sahihi? Hakumjamii.

Jibu: Kutokwa na madhiy hakuharibu swawm. Kinachoharibu swawm ni manii. Mwanaume au mwanamke akitokwa na manii ni wajibu kuilipa siku hiyo. Madhiy ni yenye kuwapata wanaume na wanawake na kwa ajili hiyo hatuwezi kusema kuwa ni wajibu kwao kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 13/06/2017