55. Dalili juu ya viganja vya Allaah 04


55- Ibn Swaa´id alisomewa: Muhammad bin ´Amr bin Hayyaan na Abu ´Utbah Ahmad bin al-Faraj ametuhadithia: Baqiyyah bin al-Waliyd ametuhadithia: Ibn Ziyaad amenihadithia, kutoka kwa Abu Umaamah (au kutoka kwa Swahabah mwengine), kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Mola wangu (´Azza wa Jall) ameniahidi kuwaingiza watu 70.000 katika Ummah wangu pasi na hesabu wala adhabu. Katika kila 1000 kuna 70.000; viganja vitatu vya Mola (´Azza wa Jall).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 09/04/2018