55. Baadhi ya fadhilah za Muhaajiruun na Answaar

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

وأنصاره والمهاجرون ديارهم

23 – Vilevile na Wanusuraji wake na Wahajiri wa miji yao

بنصرتهم عن كية النار زحزحوا

kwa unusuraji wao wameokolewa na Moto

MAELEZO

Muhaajiruun na Answaar vilevile wana fadhila kubwa. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Na wale waliotangulia awali katika Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye na amewaandalia mabustani ipitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (09:100)

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ

“Mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli.” (59:08)

Muhaajiruun ni wale waliohama kutoka Makkah kwenda al-Madiynah. Walihama kutoka katika miji yao kwa ajili ya kuunusuru Uislamu.

Answaar ni wale waliomnusuru Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakawasaidia ndugu zao katika mji wa uhamiaji. Haya yametajwa katika Suurah “al-Hashr”:

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ

“Mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli.” (59:08)

Halafu akasema kuhusu Answaar:

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Na wale waliokuwa na makazi [Madiynah] na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa [Muhaajiruun] na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe ni wahitaji. Na yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” (59:09)

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kwa unusuraji wao wameokolewa na Moto.”

Allaah amewaokoa na Moto kwa kusuhubiana kwao na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 129
  • Imechapishwa: 11/01/2024