Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

4- Hakuna chenye kumshinda.

MAELEZO

Haya yanathibitisha ukamilifu wa uwezo Wake. Amesema (Ta´ala):

لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yale yote yaliyomo humo.  Naye juu ya kila kitu ni Muweza.”[1]

وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا

”Allaah siku zote ni Mwenye uwezo wa kila jambo.”[2]

إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا

”Hakika Yeye ni Mjuzi wa yote, Muweza.”[3]

Hakuna chenye kumshinda Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Anapolitaka jambo basi husema tu “Kuwa!” na likawa. Uwezo wa Allaaah (Subhaanahu wa Ta´ala) umekizunguka na kukienea kila kitu.

Baadhi ya waandishi wanasema kuwa Allaah ni muweza kwa yale Anayoyataka. Hili ni kosa. Allaah hakufungamanisha uwezo Wake kwa utashi Wake. Amesema kwamba ni muweza juu ya kila jambo. Sema yale yaliyosemwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yaliyothibiti ni maneno Yake (Ta´ala):

وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ

“Naye kwa kuwakusanya atakapo ni Muweza.”

Kwa sababu mkusanyiko una wakati maalum huko katika mustakabali. Yeye ni muweza wa kuwakusanya huko na wakati huo wakazi wa mbinguni na ardhini. Amesema (Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ

“Miongoni mwa ishara Zake ni uumbaji wa mbingu na ardhi na aliowatawanya humo kati ya viumbe vinavyotembea – Naye kwa kuwakusanya atakapo ni Muweza.”[4]

[1] 05:120

[2] 18:45

[3] 35:44

[4] 42:29

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 12/06/2019