54. Sujuud


Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) analeta Takbiyr na anaporomoka katika Sujuud[1]. Alimwamrisha vivyo hivyo yule mtu aliyeswali kimakosa na kumwambia:

“Haitimii swalah ya yeyote mpaka… halafu aseme:

سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَه

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

mpaka asimame kwa kunyooka sawasawa. Kisha aseme:

الله أكبر

“Allaah ni mkubwa.”

halafu asujudu mpaka viungo vyake vitulizane.”[2]

Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anakusudia kwenda katika Sujuud huleta Takbiyr, akitenganisha mikono yake mbali na mbavu zake kisha ndio husujudu[3].

Wakati mwingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiinua mikono yake pindi anapoenda katika Sujuud[4].

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud na al-Haakim aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[3] Abu Ya´laa katika ”al-Musnad” (2/284) kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh na Ibn Khuzaymah (2/79/1) kwa mlolongo wa wapokezi mwingine ulio Swahiyh.

[4] an-Nasaa’iy, ad-Daaraqutwniy na al-Mukhallas katika ”al-Fawaa-id” (2/2/1) kwa isnadi mbili Swahiyh. Unyanyuaji huu umepokelewa na Maswahabah kumi. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa kitendo hicho kimewekwa katika Shari´ah. Baadhi yao ni Ibn ´Umar, Ibn ´Abbaas, al-Hasan al-Baswriy, Twaawuus na mwanae ´Abdullaah, mtumwa wa Ibn ´Umar Naafiy´, mwana wa Ibn ´Umar Saalim, al-Qaasim bin Muhammad, ´Abdullaah bin Diynaar na ´Atwaa´. ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy amesema:

”Ni Sunnah.”

Kitendo hichi kimefanywa na imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal na ni moja katika maoni ya Maalik na ash-Shaafi´iy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 121-122
  • Imechapishwa: 18/02/2017