54. Radd kwa wale wenye kutaka kufanya umoja wa dini zote

Watu hawa ambao hii leo wanafanya makongamano mbalimbali kwa ajili ya kufanya umoja wa dini. Kwa masikitiko makubwa wanasapotiwa na wale ambao wanajinasibisha na Uislamu na kuyafanya makongamano haya. Wanasema kuwa haya ni mazungumzo kati ya dini mbalimbali, mazungumzo kwa ajili ya maendeleo na mfano wa hayo. Hawafanyi makongamano hayo kwa lengo la kubadilisha shubuha za mayahudi na manaswara. Wanayafanya kwa ajili ya kupatana pamoja nao. Wametoshelezwa na kule kukubali kwao kwa nje kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume na wala hawakubali kuenea kwa ujumbe wake. Bali wanakufuru juu ya kwamba ujumbe wake ni kwa watu wote. Ni kama kwamba wanasema turidhieni na sisi tukuridhieni. Amesema (Ta´ala):

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ

“Hawatoridhika nawe mayahudi wala manaswara mpaka ufuate mila zao.” (al-Baqarah 02:120)

Wanawahadaa.

Lililo la wajibu ni kuwakufurisha na kukata kabisa juu ya ukafiri wao. Mtu asiwe na mashaka na wasiwasi juu ya ukafiri wao. Hali iendelee hivi mpaka pale watapomuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakamfuata. Amesema (Ta´ala):

فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ

“Hivyo basi, wale waliomwamini na wakamtukuza na wakamsaidia na wakafuata Nuru ambayo imeteremshwa pamoja naye… “

Je, hivi kweli wao wanafuata nuru iliyoteremshwa pamoja na Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hapana. Hawaifuati. Hata ikiwa watasema kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume, lakini hata hivyo hawamfuati. Kwa hiyo ni makafiri. Hili halina shaka. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna yeyote atakayesikia kuhusu mimi, si myahudi wala mnaswara, kisha asiamini yale niliyokuja nayo isipokuwa ataingia Motoni.”[1]

Ni lazima kukata kabisa katika kuwakufurisha makafiri. Wanaoshika msitari wa mbele kabisa ni mayahudi na manaswara. Kwa sababu wao wamemuasi Allaah kwa ujuzi. Amesema (Ta´ala):

يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖوَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Wanamtambua kama wanavyowatambua watoto wao. Na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.” (al-Baqarah 02:146)

Ni wajibu kwa waislamu kuitakidi ukafiri wa washirikina yeyote yule awaye. Kila mwenye kumshirikisha Allaah au akaomba pamoja na Allaah kwa kufanya aina yoyote miongoni mwa aina za shirki kubwa, basi ni wajibu kumkufurisha na kumhukumu ukafiri. Wala haijuzu kuwa na shaka juu ya ukafiri wao. Haijuzu kuonelea yale waliyomo kuwa ni sahihi na ya sawa na kusema: “Huyu ni mtu mwenye msimamo katika dini yake na kwamba ni bora kuliko mwenye kuabudu masanamu… ” Ukafiri ni dini moja.

Tunasema kwamba, yule ambaye hamuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na  akamfuata, basi huyo ni kafiri vyovyote iwavyo. Hii ni ´Aqiydah. Ni wajibu kwa muislamu kuitakidi namna hii ili asitoke katika Uislamu naye hajui. Anatoka katika Uislamu akiwa na shaka juu ya ukafiri wa makafiri, akaonelea kuwa dini zao ni sahihi kwa njia ya kwamba akaonelea ni sahihi yale waliyomo ndani yake mayahudi na manaswara na akasema ni watu wanaofuata dini sahihi. Bali wapo baadhi ya watu wanaojinabisha na Da´wah wanaosema ndugu zetu wanaomfuata al-Masiyh (Masihhiyyuun).

Tunawaambia kwamba watu hawa sio waumini. Lau wangelimwamini kweli basi wangelimfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu al-Masiyh amesema:

إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ

“Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu ninayesadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake “Ahmad.” (asw-Swaff 61:06)

Hawakuyaamini haya. Bali al-Masiyh atapoteremka katika zama zamwisho atamfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na atahukumu kwa Shari´ah ya Uislamu. Atakuwa ni Mujaddid miongoni mwa Mujaddiduun. Ni wajibu kuyajua mambo haya na wala mtu asidanganyike na shubuha hizi za leo ambazo zinasambazwa na mayahudi na manaswara. Wao hawataki waislamu wabaki katika dini zao. Wanachotaka ni wakuvuta waislamu katika dini zao. Amesema (Ta´ala):

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ

“Hawatoridhika nawe mayahudi wala manaswara mpaka ufuate mila zao.” (al-Baqarah 02:120)

Hivi ndivo kasema Allaah. Amesema (Ta´ala):

 وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا

“Wakasema: “Kuweni mayahudi au manaswara mtaongoka.” (al-Baqarah 02:135)

Kwa mujibu wao wanaona kuwa yule ambaye si myahudi wala mnaswara si mwongofu. Hivi ndivo kasema Allaah ambaye ni mkweli kabisa. Vipi hatuwakufurishi? Vipi tutakuwa na shaka juu ya ukafiri wao? Tunamuomba Allaah afya.

Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamewakufurisha wale wenye kumshirikisha Allaah na wakaabudu kinyume na Allaah yeyote yule awaye. Au akamkufuru Mtume miongoni mwa Mitume, akakanusha nguzo miongoni mwa nguzo sita za imani. Mtu kama huyu anahukumiwa kuwa ni kafiri na wala mtu asiwe na mashaka na wasiwasi kwa hilo na wala asionelee kuwa yale wanayofuata ni sahihi na ya sawa na akawatafutia nyudhuru na mfano wa hayo. Katika dini hakuna kupakana mafuta wala kuacha kitu cha kidini kwa sababu ya mtu mwingine. Ni wajibu kuiweka waziwazi na kujitenga mbali na yale yaliyo kinyume chake.

[1] Ameipokea Muslim (153)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 81-84
  • Imechapishwa: 06/09/2018