54. Ni ipi hukumu ya kuoga baada ya kumwaga?

Swali 54: Wanachuoni wametofautiana juu ya uwajibu wa kuoga baada ya kumwaga. Nini hukumu ya hilo?

Jibu: Ni wajibu kuoga baada ya kumwaga. Pindi mtu anapomwaga basi ni wajibu aoge. Lakini akiota bila ya kumwaga hakuna kinachomlazimu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maji yanatokamana na maji.”

Hadiyth imefutwa kwa upande mmoja na hukumu yake ni yenye kubaki kwa upande mwingine. Imefutwa kutokana na jimaa. Ni wajibu kuoga baada ya jimaa hata kama mtu hakumwaga. Dhakari ikiingia tu ndani ya tupu inakuwa ni wajibu kuoga.

Kuhusu ndoto za kimapenzi, ni wajibu kuoga pale tu ambapo mtu atamwaga. Endapo hatomwaga, basi sio wajibu kwake kuoga.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 13/06/2017