54. Nasaha za al-Khattwaab al-Makhzuumiy al-Qurashiy kwa mwanae V

1 – Ee mwanangu kipenzi! Hakika mwanamke ndiye utulivu wa mume. Hawezi kuishi pamoja naye kama wanatofautiana. Ukiwa na nia ya kumuoa mwanamke basi ulizia familia yake. Kwani mizizi mizuri huzalisha matunda mazuri.

2 – Tambua kuwa wanawake wako tofauti. Waepuke wanawake wenye maudhi. Wako wanawake ambao wanajiona na wanawadharau waume zao. Mume akimtukuza, basi huona ni kwa sababu yeye ni mtukufu kumliko. Hashukuru mazuri anayofanyiwa. Haridhiki kwa kidogo. Ulimi wake dhidi ya mume wake ni kama upanga mkali.

3 – Hajali dini wala maisha yake ya dunia. Hamtunzi kutokana na urafiki wala kutokana na wingi wa watoto. Pazia lake limeraruka na kutawanyika. Huamka asubuhi hali ya kuwa ni mwenye huzuni na inapokuwa jioni anakuwa mwenye kusimangwa. Kinywaji chake ni kichungu na chakula chake ni chenye kuchukiza. Watoto wake wamepotea. Nyumba yake imechakaa. Nguo zake ni chafu. Nywele zake zimekaa timtim.  Akicheka, basi hutwezwa. Anapozungumza, basi ametenzwa nguvu. Mchana wake ni usiku na usiku wake ni mateso. Anamuuma kama nyoka na kumdunga kama nge.

4 – Wako wanawake walio na sumu. Hugeuza kanzu zao kutegemea na upepo. Mwanamme akisema “Ndio”, wao husema “Hapana”. Akisema “Hapana”, wao husema “Ndio”. Anamdhalilisha.

5 – Wako wanawake wapumbavu. Wanacheza kimapenzi katika wakati usiofaa na huyaingilia mambo yasiyowahusu. Hayuko radhi na mapenzi yake na pato la mwanamme. Hula kama punda wa malisho. Jua huchomoza na hujamsikia amesema neno. Nyumba yake haijafagiwa. Chakula chake kimechacha. Vyombo vyake ni vyenye mafuta. Unga wake ni mchungu.

  6 – Wako wanawake wengine wenye mahaba na wenye kuvutia. Wamebarikiwa na ni wenye kuzaa sana. Ni wenye kuaminika wakati mume yuko mbali. Wanapendwa na majirani zake. Ni mwenye kusemwa vizuri anapokuwa mwenyewe na anapokuwa na wengine. Huyu ni mke mtukufu. Ni mkarimu. Ni mwenye kuzungumza kwa sauti ya chini. Nyumba yake ni safi. Mtumishi wake ni mnene. Mtoto wake wa kiume amepambwa na ni mzuri. Kheri yake ni endelevu. Mume wake anaburudika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 203-204
  • Imechapishwa: 22/08/2021