54. Dalili juu ya viganja vya Allaah 03

54- Ibn Swaa´id ametukhabarisha: Abu Ayyuub an-Nahrawaaniy ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Abdil-Jabbaar ametuhadithia: Ismaa´iyl ametuhadithia: Muhammad bin Ziyaad amenihadithia, kutoka kwa Abu Umaamah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mola wangu (´Azza wa Jall) ameniahidi kuwaingiza watu 70.000 katika Ummah wangu pasi na hesabu wala adhabu. Katika kila 1000 kuna 70.000; viganja vitatu vya Mola (´Azza wa Jall).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 104-105
  • Imechapishwa: 09/04/2018