53. Ukafiri mbaya ni wa yule mwenye kuonelea kuwa dini za washirikina ni za sawa

Baya zaidi kuliko hayo ni yule mwenye kuonelea kwamba dini yao ni sahihi. Ni wingi ulioje wa watu hii leo wenye kuonelea kuwa dini za washirikina ni za sawa na kuzitetea! Khaswakhaswa mayahudi na manaswara.

Leo hii kuna kuna propaganda zinazoenezwa kuhusu umoja wa dini tatu, kama wanavyodai; Uislamu, uyahudi na unaswara. Wanasema kuwa zote ni din. Wote wanamuamini Allaah. Kwa ajili hiyo hawaonelei kuwa ni makafiri. Huyu ni mwenye ukafiri mbaya zaidi kuliko yule mwenye mashaka juu ya ukafiri wao. Kwa sababu huyu ameonelea kuwa dini zao ni za sawa na kwamba wanamuamini Allaah na kwamba eti wanawafuata Mitume. Wanasema kuwa mayahudi wanamfuata Muusa na manaswara wanamfuata ´Iysaa. Tunawaambia kuwa ni waongo. Hawakumfuata Muusa wala ´Iysaa. Lau kweli wangelikuwa wanamfuata Muusa na ´Iysaa, basi wangelimwamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu Muusa na ´Iysaa (´alayhimaas-Salaam) wanabashiria ujio wa Muhammad. Isitoshe ametajwa katika Tawraat na Injiyl. Tawraat iliokuja na Muusa ametajwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ

“… ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl.” (al-A´raaf 07:157)

Vivyo hivyo Injiyl ambayo imeteremshwa kwa ´Iysaa ametajwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali ´Iysaa aliweka hilo wazi kabisa. Alisema:

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ

“Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu ninayesadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake “Ahmad.” (asw-Swaff 61:06)

Ni nani aliyekuja baada ya ´Iysaa? Ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama majina mengi. Amesema (Ta´ala):

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖوَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Wale ambao Tumewapa Kitabu wanamtambua kama wanavyowatambua watoto wao. Hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.” (al-Baqarah 02:146)

Kwa hivyo yule asiyeingia katika Uislamu na akamuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kafiri. Haijalishi kitu kama atakuwa ni myahudi, mnaswara, mwabudu kaburi au mkanamungu. Inahusiana na kila yule ambaye hamuamini Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huyo ni kafiri.Vipi basi mtu atalinganisha baina ya uyahudi, unaswara na Uislamu? Uyahudi na unaswara baada ya kutumilizwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zimefutwa kwa Uislamu. Uislamu ndio dini ya haki.  Baada ya kutumwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hapakubaki dini sahihi zaidi ya Uislamu aliokuja nao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 06/09/2018