53. Uasi na vita kwa mtawala haijuzu

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Si halali kumpiga vita mtawala. Asiwepo mtu yeyote atakayemfanyia uasi. Atakayefanya hivo basi ni mtu wa Bid´ah aliye mbali na Sunnah na njia iliyonyooka.”

MAELEZO

Kwa sababu kumfanyia uasi mtawala ni kwenda kinyume na dalili zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni moja katika misingi mikubwa ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Midhali huna uwezo na madhara ni makubwa kuliko manufaa, basi hupaswi hata kumfanyia uasi kafiri. Pale utapokuwa na uwezo na kukawa kuna manufaa makubwa kuliko madhara ndio itakuwa inajuzu. Vinginevyo inatakiwa kusubiri. Lakini midhali mtawala ni muislamu na anaswali, hivyo basi itakuwa haifai kumfanyia uasi mpaka pale atakapoonyesha kufuru ya wazi kabisa. Hapo ndipo anatakiwa kukabiliwa kwa masharti yaliyotajwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 425
  • Imechapishwa: 02/12/2017