53. Sura ya tano: Ubainifu wa ukweli kuhusu na kuritadi, aina zake na hukumu zake

4- Kuritadi: Kilugha maana yake ni kurejea. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ

“Wala msirejei kugeuka nyuma kukimbia [kupigana] mtageuka kuwa wenye kukhasirika.”[1]

Bi maana msirejei

Kuritadi katika istilahi ya Kishari´ah maana yake ni ukafiri baada ya Uislamu. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

“Atakayeritadi miongoni mwenu kutoka dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao yameporomoka matendo yao katika dunia na Aakhirah na hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.”[2]

Vigawanyo vyake

Kuritadi kunatokea kwa kutendeka  moja katika vichenguzi vya Uislamu. Vichenguzi vya Uislamu ni vingi na vyote vinarejea katika vigawanyo vinne ambavyo ni vifuatavyo:

1- Kuritadi kwa maneno: Ni kama kumtukana Allaah (Ta´ala), kumtukana Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Malaika Zake, mmoja katika Mitume Yake, kudai kwamba mtu anajua elimu iliyofichikana, kudai utume au kumsadikisha mwenye kuudai, kumuomba asiyekuwa Allaah, kumtaka msaada katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah au kumtaka ulinzi katika jambo hilo.

2- Kuritadi kwa kitendo: Kulisujudia sanamu, mti, jiwe, kaburi, kulichinjia, kuutupa msahafu sehemu ya taka, kufanya uchawi, kujifunza nao au kuufunza au kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah na wakati huohuo mtu akaona kuwa inafaa.

3- Kuritadi kwa kuamini. Kama mtu kuamini kuwa Allaah ana mshirika, kwamba uzinzi, pombe na ribaa ni halali, mkate ni haramu, swalah sio lazima na mfano wa hayo miongoni mwa vitu ambavyo kuna maafikiano juu ya uhalali wake, uharamu wake au uwajibu wake. Inahusiana na vile vitu ambavo kuna maafikiano ya kukata kabisa na mtu mfano wake hayajahili.

4- Kuritadi kwa kutilia mashaka katika kitu chochote vilivyotangulia. Ni kama mfano  wa mwenye kutilia mashaka juu ya uharamu wa shirki, uharamu wa uzinzi na pombe, uhalali wa mkate, akawa na mashaka juu ya ujumbe wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ujumbe wa Nabii yeyote mwengine, kuhusu ukweli wake, kuhusu dini ya Uislamu au kwenda kwake na wakati katika zama hizi.

5- Kuritadi kwa kuacha: Ni kama mfano wa mwenye kuacha swalah kwa makusudi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mja na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”[3]

Zipo dalili nyenginezo zinazothibitisha ukafiri wa mwenye kuacha swalah.

[1] 05:21

[2] 02:217

[3] al-Bukhaariy (3017) na Muslim (242).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 19/03/2020