Swali 53: Je, inafaa kufupika na moja kati ya Suurah mbili ambazo ni Suurah “as-Sajdah” na “al-Insaan” katika Fajr ya ijumaa[1]?

Jibu: Sunnah ni kuzisoma zote mbili na asifupilizike na moja wapo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”[2]

Vilevile kutokana na ueneaji wa maneno Yake (´Azza wa Jall):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

 “Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah.”[3]

Jengine ni kwamba kufanya hivo kunaihuisha Sunnah na kuihifadhi.

MWISHO!

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/397).

[2] al-Bukhaariy (631) na ad-Daarimiy (1253).

[3] 33:21

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 106
  • Imechapishwa: 10/12/2021