53. Ni lipi linalomlazimu mtu aliyepata khabari kuingia kwa Ramadhaan mida ya asubuhi?

Swali 53: Kuna mtu Ramadhaan imeingia na akaja kupata khabari mida ya asubuhi. Ni lipi linalomlazimu?

Jibu: Baada ya kupata khabari kuwa ni Ramadhaan ni wajibu kwake kujizuia na kula na kunywa na kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 13/06/2017