53. Nguzo ya nne: Rukuu´


Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Halafu mtu anaenda kwenye Rukuu´, kuinuka kutoka kwenye Rukuu´, kunyooka sawasawa, kusujudu juu ya viungo saba na kuinuka kutoka hapo na kukaa baina ya Sajdah mbili. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا

“Enyi mloamini! Rukuuni na sujuduni.”[1]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimeamrishwa kujusudu juu ya viungo saba.”[2]

MAELEZO

Maneno yake:

“Nguzo ya nne miongoni mwa nguzo za swalah ni Rukuu´.”

Maana ya Rukuu´ ni kuinama, kuweka mikono yako kwenye magoti yako, kuachanisha vidole vyako na kuutandaza na kuuweka sawa mgongo wako na useme:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

Ambaye hatosema hivo swalah yake haitosihi.

[1] 22:77

[2] al-Bukhaariy (810) na Muslim (490).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 87
  • Imechapishwa: 21/06/2022