53. Kuzungumza maneno mazuri juu ya Maswahabah wote

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

وقل خير قولٍ في الصحابة كلِّهم

19 – Zungumza maneno mazuri juu ya Maswahabah wote

ولا تك طعَّاناً تعيبُ وتجرحُ

     usiwe ni mtusi kazi yako ni kutia aibu na kujeruhi

فقد نطقَ الوحيُ المبين بفضلِهم

20 – Wahy wenye kubainisha umezitamka fadhilah zao,

وفي الفتح آيٌ للصَّحابةِ تمدحُ

     na katika “al-Fath” kuna Aayah inayowasifu

MAELEZO

Alipowataja waliobakia baada ya kuwataja wale kumi waliobashiriwa Pepo ndio akasema:

“Zungumza maneno mazuri.”

ili isije kudhaniwa kwamba akitajwa yule Swahabah ambaye ni mbora zaidi ina maana ni kumtukana yule ambaye anashindwa ubora. Wote ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wana fadhilah za usuhubiano na kumnusuru Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walipokea kutoka kwake, wamepokea kutoka kwa Mtume, wakamuamini, wakakusanyika naye, wakaswali nyuma yake na wakamsikia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“… kwa Maswahabah wote.”

Bi maana Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wasifu kwa sababu wanastahiki sifa hizi.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Usiwe ni mtusi kazi yako ni kutia aibu na kujeruhi.”

Haijuzu kumtukana yeyote katika wao au kuzitaja aibu zao. Hivi ndivyo wanavyofanya Raafidhwah Allaah awatweze. Wao ni maadui wa dini, maadui wa Ummah na ni maadui wa Uislamu. Hivi vilevile ndivyo wanavyofanya Khawaarij ambao wamewakufurisha Maswahabah.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wahy wenye kubainisha umezitamka fadhilah zao.”

Wahy unakusanya Qur-aan na Sunnah. Wahy, ambao ni Qur-aan na Sunnah, umezitaja fadhilah za Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ambaye anawatukana ni mwenye kukadhibisha Qur-aan na Sunanh za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Na wale waliotangulia awali katika Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye na amewaandalia mabustani ipitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (09:100)

Katika Suurah “al-Fath” ambayo inaanza kwa:

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا

“Hakika tumekufungulia Ushindi ambao ni wa wazi.” (48:01)

kumetajwa sifa zenye kukariri juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwanzoni mwake amesema (Ta´ala):

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا

“Ili Awaingize waumini wa kiume na waumini wa kike [ndani ya] mabustani yapitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele – na Awafutie maovu yao na limekuwa hilo mbele ya Allaah, ni kufuzu kukubwa.” (48:05)

إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚفَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا

“Hakika wale waliofungamana ahadi ya utiifu nawe, hakika hapana vyengine isipokuwa wanafungamana ahadi ya utiifu na Allaah. Mkono wa Allaah uko juu ya mikono yao. Basi atakayevunja [fungamano hilo], hakika hapana isipokuwa anavunja dhidi ya nafsi yake na yeyote atimizaye yale aliyomuahidi Allaah, basi Atampa ujira mkubwa.” (48:10)

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ

“Hakika Allaah amewawia radhi waumini waliokupa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti. Alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao, basi Akawateremshia utulivu na akawalipa ushindi wa karibu.” (48:18)

Mwishoni mwake akasema:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖسِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni wasifu wao… “

 Bi maana sifa zao:

فِي التَّوْرَاةِ

“… katika Tawraat…. “

Ambayo aliteremshiwa Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam).

وَمَثَلُهُمْ

“… na ni wasifu wao…. “

Bi maana sifa zao:

فِي الْإِنجِيلِ

“… katika Injiyl… “

Ambayo aliteremshiwa ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam).

كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا

“… kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili liwaghadhibishe makafiri. Allaah amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkubwa.” (48:29)

Hizi ndio sifa zao zilizomo katika Tawraat na Injiyl.

Amesema (Ta´ala):

لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“… ili liwaghadhibishe makafiri.” (48:29)

Ni dalili inayofahamisha kuwa yule anayewachukia au kuwabughudhi Maswahabah ni kafiri. Kutokana na andiko la Aayah hii tukufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 124-126
  • Imechapishwa: 10/01/2024