54- Kuhusu kuyabeba majeneza juu ya marikwama au magari maalum kwa ajili ya mazishi na yakasindikizwa na wale wenye kuyasindikiza na wao wamo ndani ya magari yao, sura kama hii haikubaliki kabisa. Hilo ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:

La kwanza: Ni katika desturi za makafiri. Ni jambo limethibiti katika Shari´ah kwamba haijuzu kuwafuata katika mambo hayo. Kumepokelewa Hadiyth nyingi sana juu ya jambo hilo. Nimezichunga na nimezitoa katika kitabu changu “Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah fiy-Kitaab as-Sunnah”. Baadhi yake zinaamrisha na kuhimiza kwenda kinyume nao katika ´ibaadah zao, sera zao na desturi zao.  Baadhi ya zingine ni katika matendo yake yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kuwakhalifu katika jambo hilo. Yule anayetaka kukisoma basi akirejelee.

La pili: Ni Bid´ah katika ´ibaadah pamoja na kwamba ni kitu kinapingana na Sunnah ya kimatendo katika kubeba jeneza. Kila ambacho ni hivo katika mambo yaliyozuliwa basi ni upotevu kwa makubaliano.

La tatu: Ni kujikosesha lengo katika kubeba na kusindikiza. Isitoshe ni jambo linamkumbusha mtu Aakhirah. Hayo yamesemwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth iliotangulia mwanzoni mwa kipengele hichi kwa tamko lisemalo:

 “… na yafuateni majeneza kutakukumbusheni Aakhirah.”

Hakika kuyasindikiza kwa sura kama hiyo ni miongoni mwa mambo yanayowakosesha watu lengo hili tukufu ukoseshaji kamili au chini ya hivo. Ni jambo lisilofichika kwa kila mwenye macho kwamba kumbeba maiti juu ya mabega na wasindikizaji wakaliona wakati linapokuwa juu ya vichwa vyao ni jambo linalohakikisha zaidi kukumbuka na wakawaidhika juu ya sura iliyotajwa. Sintokuwa mwenye kuchupa mipaka nikisema kwamba kile kilichowafanya wazungu kufanya hivo ni kuogopa kwao kufa na kila kinachokumbushia jambo hilo. Yote hayo ni kwa sababu ya kughilibiwa na ulimwengu na kuikufuru kwao Aakhirah.

Ya nne: Ni sababu yenye nguvu inayowapunguza wale wenye kulisindikiza na wenye kutaka kufikia ujira ambao umetangulia kutajwa katika masuala ya 45 katika kipengele hichi. Hivo ni kwa sababu si kila mmoja anao uwezo wa kukodisha gari ili aweze kulisindikiza.

Ya tano: Sura hii haiafikiani si kwa karibu wala kwa mbali pamoja na yale yanayotambulika katika Shari´ah safi katika kuepuka shakili na michoro na khaswa katika jambo kama hili la khatari ambalo ni kifo. Nasema kwa haki kwamba endapo katika Bid´ah hii kusingelikuwa na jengine isipokuwa mukhalafa huu, basi ingelitosha katika kuikataa. Tusemeje kukijumuishwa juu yake yale yaliyotangulia kutajwa katika mambo yanayokwenda kinyume, maharibifu na mengineyo ambayo siyakumbuki?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 99-101
  • Imechapishwa: 14/07/2020