53. Kufaa kumuozesha msichana mdogo kwa mwanamume mkubwa

1 – Kuhusu msichana ambaye ni mdogo bikira hakuna tofauti kwamba inafaa kwa baba yake kumuozesha bila idhini yake. Kwa sababu yeye hana idhini. Kwa sababu Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alimuozesha msichana wake ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku ni msichana wa miaka sita na akamwingilia akiwa na miaka tisa. Imaam ash-Shawkaaniy amesema katika “Nayl-ul-Awtwaar”:

“Katika Hadiyth kuna dalili inayoonyesha kwamba inafaa kwa baba kumuozesha msichana wake kabla ya kubaleghe.” Amesema tena: “Pia kuna dalili inayofahamisha kwamba inafaa kumuozesha msichana mdogo kwa mwanaume mkubwa. al-Bukhaariy ameliwekea hilo mlango na akataja Hadiyth ya ´Aaishah na katika “al-Fath” kumetajwa maafikiano juu ya hilo.”[1]

Mtunzi wa “al-Mughniy” amesema:

“Ibn-ul-Mundhir amesema: “Wameafikiana wale wanachuoni wote ambao tumehifadhi kutoka kwao kwamba baba kumuozesha msichana wake mdogo inajuzu ikiwa ameolewa na mtu mwema.”[2]

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) kumuozesha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akiwa ni msichana wa miaka sita, kuna Radd kali kwa wale ambao wanapinga kumuozesha msichana mdogo kwa mtu mkubwa, wanafanya kitendo hicho kuwa kibaya na cha maovu. Haya ni kwa sababu ya ujinga wao au kwamba ni wapuuzi.

[1] (06/128-129).

[2] (06/487).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 19/11/2019