´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwatukane maiti. Kwani wameshayaendea yale waliyoyatanguliza.”

Ameipokea Imaam Ahmad, al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy.

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwatukane maiti wetu mkaja kuwaudhi waliohai wetu.”

Ameipokea Ahmad.

Abu Raafiy´ Aslam mtumishi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza akuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumwosha maiti kisha akamsitiri Allaah humsamehe mara arubani.”

Ameipokea al-Haakim aliyesema:

“Ni Swahiyh kwa masharti ya Muslim.”

Ibn-us-Simaak amesema:

“Upande ni ule ulio kinywani mwako. Unakula kila kinachopita mbele yako. Umewaudhi watu wote katika mji na hivi sasa umewaendea waliyo ndani ya makaburi. Nyuso za waliyo ndani ya makaburi zimetiwa kwenye mtihani na wewe umesimama hapa na kuwachimbua. Maiti huchimbuliwa pindi anaposemwa vibaya. Hufai kumsema vibaya ndugu yako kwa sababu tatu. Huenda ukamsema vibaya kwa kitu ambacho na wewe uko nacho. Pili huenda ukamsema vibaya kwa kitu ambacho Allaah wewe amekusalimisha nacho. Hivo ndivyo unavyomshukuru Yule aliyekusalimisha? Hujasikia namna inavyosemwa kuwa unatakiwa kumrehemu nduguyo na umshukuru Yule aliyekusalimisha wewe?”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 22/10/2016