53. Dalili juu ya viganja vya Allaah 02


53- Abu Muhammad bin Swaa´id alisomewa: Muhammad bin Harb ametuhadithia Waasitw: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ziyaad, kutoka kwa Abu Umaamah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mola wangu (´Azza wa Jall) ameniahidi kuwaingiza watu 70.000 katika Ummah wangu pasi na hesabu wala adhabu. Katika kila 1000 kuna 70.000; viganja vitatu vya Mola (´Azza wa Jall).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 104
  • Imechapishwa: 09/04/2018