53. Allaah anazumgumza na sisi tunazungumza

Viumbe wanazumgumza na Allaah (Jalla wa ´Alaa) anazungumza. Viumbe wanasikia na Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasikia. Viumbe wanaona na Allaah (Jalla wa ´Alaa) anaona. Lakini sifa za Allaah zinalingana Naye na sifa za viumbe zinalingana nao. Hazifanani. Sifa za viumbe zimeumbwa tofauti na sifa Zake ambazo hazikuumbwa na ni za milele na zisizokuwa na kikomo. Maneno Yake hayaishi na wala hayana kikomo. Amesema (Ta´ala):

قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا

“Sema: “Endapo bahari ingelikuwa ni wino wa [kuandika] maneno ya Mola wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu ijapo tungelileta mfano wake kujaza tena.”[1]

وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

”Na lau kama miti yote iliyomo ardhini ingekuwa ni kalamu na bahari [ikawa wino], na ikaongezewa juu yake bahari zengine saba, basi yasingelimalizika maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika,  Mwenye hekima ya yote.”[2]

Allaah anazungumza akitaka, huzungumza milele na huzungumza huko mustakabali. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anaamrisha, anakataza na anaendesha mambo. Maneno Yake hayana kikomo. Alimzungumzisha Jibriyl na Jibriyl akayaskia maneno Yake. Alimzungumzisha Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Muusa akayasikia maneno Yake. Usiku wa safari ya kupandishwa mbinguni alimzungumzisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alimzungumzisha Aadam.

Kwa hivyo Allaah anazungumza kwa maneno yanayolingana na utukufu Wake (Jalla wa ´Alaa). Maneno Yake hayafanani na maneno ya viumbe kama ambavo sifa Zake nyenginezo zote hazifanani na sifa za viumbe:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[3]

[1] 18:109

[2] 31:27

[3] 42:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 02/08/2021