53. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kwanza wa Aal ´Imraan


al-´Ayyaashiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ

“Yeye ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu, humo mna Aayaat zilizo wazi kabisanazo ndio msingi wa Kitabu – na nyinginezo haziko wazi.”[1]

“´Abdur-Rahmaan bin Kathiyr al-Haashimiy amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema:

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ

“Yeye ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu, humo mna Aayaat zilizo wazi kabisa… “

“Ni kiongozi wa waumini na maimamu.”

وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ

“… na nyinginezo haziko wazi.”

Ni fulani na fulani:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ

“Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu… “

Ni wafuasi wao na wale wenye kusimama upande wao:

فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ

“… hufuata zile zisizokuwa wazi ili kutafuta fitnah na kutafuta kuzipotosha.”[2]

Tafsiri hii ni kumzulia Allaah (´Azza wa Jall) uongo, kupotosha Kitabu Chake na kipingamizi cha wazi dhidi ya andiko la Qur-aan. Allaah anamwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ

“Yeye ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu, humo mna Aayaat zilizo wazi kabisa…

Ni zile Aayah zilizo wazi na bayana ambazo ndio msingi wa Qur-aan. Amesema vilevile:

وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ

“… na nyinginezo haziko wazi.”

Ni baadhi ya Aayah za Qur-aan ambazo maana yake haiko wazi kwa baadhi ya watu. Mfumo sahihi ni kuzipeleka zisizo wazi kwa zilizo wazi. Anayefanya hivo amefuata njia ya sawa na ameepuka matamanio. Baatwiniyyah hawa wanacheza na Aayah za Qur-aan zilizo wazi na wanazifasiri kwa matamanio yao. Vivyo hivyo ndivyo wanavyofanya na Aayah zisizo wazi. Wanafasiri Aayah zisizokuwa wazi kwa njia ya watu na kusema kuwa ni Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan. Hili ni kujengea juu ya kwamba wanaonelea kuwa ni makafiri. Haya ni katika tafsiri mbaya kabisa ya Baatwiniyyah – Allaah awafedheheshe!

[1] 03:07

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/162).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 85
  • Imechapishwa: 03/04/2017