3- Upotevu: Kupondoka kutoka katika njia iliyonyooka ambako ni kinyume na uongofu. Amesema (Ta´ala):

مَّنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا

“Anayeongoka, basi ameongoka kwa ajili ya manufaa ya nafsi yake na anayepotoka, basi amepotoka kwa khasara yake.”[1]

Kunasemwa upotevu na kunakusudiwa maana nyingi:

1- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa ukafiri. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Yake na siku ya Mwisho, basi hakika amepotoka upotofu wa mbali.”[2]

2- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa shirki. Amesema (Ta´ala):

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ

“Lakini Allaah anayashuhudia aliyoyateremsha kwako [kwamba] ameyateremsha kwa ujuzi Wake na Malaika pia wanashuhudia na Allaah anatosheleza kuwa Mwenye kushuhudia yote.”[3]

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali.”[4]

3- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa wendaji kinyume ulio chini ya kufuru. Kama inavosemwa ´kundi potevu` bi maana linalokwenda kinyume.

4- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa kosa. Miongoni mwa hayo ni maneno ya Muusa (´alayhis-Salaam):

فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ

“Nilikifanya hapo pindi nilikuwa miongoni mwa waliokosea.”[5]

5- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa kusahau. Miongoni mwa hayo ni maneno Yake (Ta´ala):

أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ

”… ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akisahau, basi mmoja wao atamkumbusha mwengine.”[6]

6- Mara husemwa hivo na kukakusudiwa upotezaji na kutokuwepo. Miongoni mwa hayo ni ´ngamia amepotea`[7].

[1] 17:15

[2] 04:136

[3] 04:116

[4] 04:116

[5] 26:20

[6] 02:282

[7] al-Mufradaat, uk. 297-298 cha ar-Raaghiyb al-Aswfahaaniy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 18/03/2020