Ee dada wa Kiislamu! Fanya haraka kuolewa muda wa kuwa ni dada mwenye kutakiwa. Usicheleweshe kwa sababu ya kuendelea na masomo au kufanya kazi. Wala kuolewa hakuwekewi badali na masomo wala kazi vovyote itavyofikia. Simamia kazi za nyumbani kwako na kuwalea watoto wako. Kwani hii ndio kazi yako ya kimsingi na matunda ya maisha yako. Usitafute badala yake. Kwani hailinganishwi na kitu. Usikose kuolewa na mwanaume mwema. Kwani hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapokujieni yule mnayeridhia kwake dini na tabia yake basi muozesheni. Msipofanya hivo kutakuwa fitina ardhini na ufisadi mkubwa.”

Ameipokea at-Tirmidhiy na akaifanya kuwa nzuri. Ina shawaahid zengine.

Msichana ambaye anakusudiwa kuolewa hatoki nje ya hali tatu:

1 – Mdogo bikira.

2 – Amekwishabaleghe bikira.

3 – Mtumzima amekwishawahi kuolewa.

Kila mmoja katika hao ana hukumu zake maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 18/11/2019