52. Ni ipi hukumu ya anayekula na kunywa kwa kukusudia mchana wa Ramadhaan?

Swali 52: Ni ipi hukumu ya mwenye kula na kunywa katika mchana wa Ramadhaan ilihali yuko na afya njema? Ni lipi linalomlazimu?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kula na kunywa katika mchana wa Ramadhaan ilihali yuko na afya njema. Ni wajibu kwake kujizuia na kula na kunywa na ni wajibu kwake kulipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 70
  • Imechapishwa: 13/06/2017