52. Namna hii ndivo walivyoamini maimamu mashariki na magharibi

Kuna Hadiyth nyingi zinathibitisha mkono wa Allaah. Hapa kunafuatia baadhi ya maneno ya maimamu kuhusu mtu anatakiwa achukue msimamo gani juu ya sifa za Allaah (´Azza wa Jall):

54- Baqiyyah ameeleza kwamba al-Awzaa´iy amesema:

“az-Zuhriy na Mak-huul walikuwa wakisema: “Zipitisheni Hadiyth hizi kama zilivyokuja.”

55- al-Waliyd bin Muslim amesimulia:

“Nilimuuliza Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy, al-Layth bin Sa´d na al-Awzaa´iy kuhusu Hadiyth zinazoongelea sifa. Wakasema: “Zipitisheni kama zilivyokuja.”

56- al-Laalakaa´iy amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy, mwanafunzi wa Abu Haniyfah, ambaye amesema:

“Wanachuoni wote Mashariki na Magharibi wameafikiana juu ya kuamini Qur-aan na Sunnah zilizopokelewa na wapokezi waaminifu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu sifa za Mola (´Azza wa Jall) pasi na tafsiri, kuzielezea wala kuzifananisha. Yule mwenye kufasiri kitu katika hayo basi ametoka juu ya yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amefarikiana na mkusanyiko. Yule mwenye kusema yale yaliyosemwa na Jahm basi amefarikiana na mkusanyiko. Kwa sababu amemweleza kwa sifa isiyokuwa chochote.”

57- al-Awzaa´iy amesema:

“Lazimiana na mapokezi ya waliotangulia japokuwa utakataliwa na watu. Na tahadhari na maono ya watu japokuwa watakupambia kwa maneno.”

58- Imepokelewa kwamba al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Mutwarrif amezungumza maneno ambayo hayajasemwa na yeyote kabla wala baada yake. Wakasema: “Amesema nini, ee Abu Sa´iyd?” Akasema: “Shukurani zote njema anastahiki ambaye miongoni mwa kumuamini ni kuwa mjinga juu ya yale aliyojisifu nafsi Yake.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 14/07/2019