52. Maneno ya Taabi´uun kuhusu ujuu wa Allaah

68 – Muhammad ametuhadithia: Ahmad bin al-Hasan ametukhabarisha: Abul-Qaasim bin Bishraan ametuhadithia: Abul-Fadhwl bin Khuzaymah ametuhadithia: Muhammad bin Abiyl-´Awaam ametuhadithia: Muusa bin Daawuud ametuhadithia: Abu Mas´uud al-Jarraar ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin al-Aqmar ambaye amesema:

“Masruuq alipokuwa akihadithia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa daima akisema: “Amenihadithia mimi mwanamke mkweli mno, msichana wa mwanamme ambaye naye ni mkweli mno, kipenzi wa mpenzi wa Allaah, mwanamke ambaye alitakaswa kutoka juu ya mbingu ya saba. Sikumkadhibisha.”[1]

69 – Muhammad ametukhabarisha: Hamd ametuhadithia: Ahmad ametuhadithia: Abu Muhammad bin Hayyaan ametuhadithia: al-Waliyd bin Abaan ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad bin Zakariyyaa ametuhadithia: Salamah bin Shabiyb ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Hakam ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa ´Ikrimah aliyesema:

“Wakati mtu mmoja alipokuwepo kwenye bustani lake akafikiria pasi na kutikisa midomo: “Kama Allaah angeliacha nikapanda kwenye bustani. Tahamaki Malaika wakasimama kwenye mlango wa bustani lake, wameshikana mikono, wakasema: “Amani ya Allaah iwe juu yako.”Akasimama ambapo wakamwambia: “Mola wako anakwambia: “Tamani ukitakacho moyoni mwako Mimi nimekijua.”Ametuagiza kuja na mbegu hizi. Anasema: “Zipande!” Hivyo akazitupa kuliani na kushotoni, mbele yake na nyuma yake, wakawa wakubwa kama mlima, kama alivokuwa anatamani na kutaka. Ndipo Mola wake (´Azza wa Jall) akasema kutoka juu ya ´Arshi Yake: “Kula, ee mwanaadamu! Kwani hakika mwanaadamu hashibi.”[2]

70 – Nilimsomea Ahmad bin al-Mubaarak: Thaabit bin Bundaar ametukhabarisheni: Abu ´Aliy bin Duumaa ametuhadithia: Makhlad bin Ja´far ametuhadithia: al-Hasan bin ´Aliy al-Qattwaan ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Iysaa al-´Attwaar ametuhadithia: Ishaaq bin Bishr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Bakr al-Hudhaliy, kutoka kwa al-Hasan aliyesema:

“Hakuna kiumbe yeyote aliye karibu kwa Mola wako kama Israafiyl. Kati yake na Mola wake kuna pazia saba. Kila pazia umbali wake ni miaka 500. Israafily ndiye aliye chini yao. Kichwa chake kiko chini ya ´Arshi na miguu yake iko chini ya ardhi ya saba.”[3]

71 – Muhammad ametukhabarisha: Hamd ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdillaah ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin al-Fadhwl ametuhadithia: Abul-´Abbas as-Sarraaj ametuhadithia: ´Abdullaah bin Abiyz-Zinaad na Haaruun ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: Ja´far ametuhadithia: Nilimsikia Maalik bin Diynaar akisema:

“Wale ambao ni wakweli mno wanaposomewa Qur-aan, nyoyo zao zinaanza kugonga kwa ajili ya Aakhirah. Chukua, usome na sema: “Sikiliza maneno ya Mkweli kutoka juu ya ´Arshi Yake.”[4]

72 – Ahmad amesema: Baba yangu amenihadithia: Ahmad bin Muhammad bin ´Umar ametuhadithia: Abu Bakr bin ´Ubayd ametuhadithia: Abu ´Aliy al-Madaa-iniy amenihadithia: Ibraahiym bin al-Hasan ametuhadithia, kutoka kwa mzee wa ki-Quraysh ambaye Kun-yah yake ni Abu Ja´far, kutoka kwa Maalik bin Diynaar aliyesema:

“Nimesoma katika baadhi ya vitabu kwamba Allaah (´Azza wa Jall) anasema: “Ee mwanaadamu! Kheri Yangu inakuteremkia na shari yako inapanda Kwangu. Najipendekeza kwako kwa neema mbalimbali na unajichukiza Kwangu kwa maasi. Malaika mkarimu haachi kupanda Kwangu kutoka kwako akiwa na matendo maovu.”[5]

73- Ibn ´Abdil-Barr amesema:

“Sunayd  ametaja kutoka kwa Muqaatil, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Muzaahim ambaye amesema kuhusu maneno ya Allaah (Ta´ala):

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[6]

“Yeye (Tabaaraka wa Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi Yake na ujuzi Wake umeenea kila mahali.”

Nimefikiwa na khabari kwamba Sufyaan ath-Thawriy amesema mfano wake.”[7]

74 – ´Abdullaah bin Muhammad ametukhabarisha: Ahmad bin ´Aliy ametuhadithia: Hibatullaah ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad bin al-Qaasim ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Mahmuud bin Yahyaa ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Swadaqah ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan ametuhadithia: Yahyaa bin Aadam ametuhadithia, kutoka kwa Ibn ´Uyaynah aliyesema:

“Rabiy´ah aliulizwa kuhusiana na:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ‘Arshi.”[8]

Amelingana vipi?”

Akajibu:

“Kulingana ni jambo lisilokosa kutambulika. Namna haijulikani. Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni wajibu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufikisha na ni wajibu kwetu kusadikisha.”[9]

75 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Bakr ametuhadithia: Abul-Qaasim ametuhadithia: Ahmad bin ´Ubayd ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Ahmad bin Abiy Khaythamah ametuhadithia: Haaruun bin Ma´ruuf ametuhadithia: Dhwamrah bin Swadaqah ametuhadithia: Nimemsikia Sulaymaan at-Taymiy akisema:

“Nikiulizwa ni wapi alipo Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), basi nitasema kwamba yuko mbinguni.”

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.” (al-´Uluww, uk. 71)

[2] adh-Dhahabiy amesema:

” Cheni ya wapokezi wake haina jipya.” (al-´Uluww, uk. 96)

[3] adh-Dhahabiy amesema

”Abu Bakr al-Hudhaliy ni dhaifu sana.” (al-´Uluww, uk. 93)

[4] Hilyat-ul-Awliyaa’ (2/358). adh-Dhahabiy amesema:

”Hadiyth katika ”al-Hilyah” ina mlolongo wa wapokezi Swahiyh.” (al-´Uluww, uk. 97)

al-Albaaniy amesema:

”Ni jambo linalohitaji kuangaliwa vizuri.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 131)

[5] adh-Dhahabiy amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni yenye giza.” (al-´Uluww, uk. 97)

[6] 58:07

[7] at-Tamhiyd (7/139-142).

[8] 20:05

[9] Ibn Taymiyyah amesema:

”Jawabu hili limethibiti kutoka kwa Rabiy´ah, mwalimu wa Maalik.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (5/365))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 160-165
  • Imechapishwa: 05/07/2018