52. Haijuzu kufanya uasi dhidi ya viongozi wa Kiislamu

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yule anayefanya uasi dhidi ya kiongozi wa waislamu ambaye watu wamekusanyika juu yake na wakakubali ukhaliyfah wake kwa njia yoyote ile, kwa kuridhia au kwa nguvu, amewatawanyisha waislamu na ameenda kinyume na mapokezi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfanya uasi huyu akifa katika hali hii, basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”

MAELEZO

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kufa na hakuna katika shingo yake kiapo cha usikivu basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”[1]

“Yule mwenye kutoka katika utiifu basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”[2]

Haijuzu kufanya uasi. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyasema haya katika ukhaliyfah wa Yaziyd. Mnaijua hali ya Yaziyd. Pamoja na hivo Ibn ´Umar alikuwa anaonelea kuwa yule mwenye kufanya uasi dhidi yake amevunja kiapo cha usikivu na hivyo akifa katika hali hiyo basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri[3].

[1] Muslim (1851).

[2] Muslim (1848).

[3] Muslim (1851).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 424
  • Imechapishwa: 02/12/2017