52. Dalili juu ya viganja vya Allaah

52- Abu Muhammad bin Swaa´id alisomewa na mimi huku nasikiliza: al-Hasan bin ´Arafah ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ziyaad: Nimemsikia Abu Umaamah akisema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mola wangu (´Azza wa Jall) ameniahidi kuwaingiza watu 70.000 katika Ummah wangu pasi na hesabu wala adhabu. Katika kila 1000 kuna 70.000; viganja vitatu vya Mola (´Azza wa Jall).”[1]

[1] at-Tirmidhiy (2437), Ibn Maajah (4286), Ahmad (5/268), Ibn Abiy ´Aaswim (589), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr (7520) na al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (723). at-Tirmidhiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri na geni.”

Ibn Kathiyr amesema:

”Mlolongo wa wapokezi ni mzuri.”  (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (1/513))

Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (02/282)

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 103
  • Imechapishwa: 04/04/2018