Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tafsiri inayoweka wazi haya, ni maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Na kumbuka Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najivua jukumu lote kutokamana na yale mnayoyaabudu, isipokuwa Yule aliyeniumba, basi hakika Yeye ataniongoa!” Na akalifanya neno hilo ni lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.” (az-Zukhruf 43 : 26-28)

MAELEZO

Ibraahiym – Ibraahiym ndiye rafiki wa karibu wa Allaah na kiongozi wa wapwekeshaji. Yeye ndiye Mtume bora baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baba yake ni Aazar.

Najitenga mbali – Ni kitenzi kinachotokana na kujitenga mbali. Maneno yake “Hakika mimi najivua jukumu lote kutokamana na yale mnayoyaabudu” yanaafikiana na “hapana mungu wa haki… “

Isipokuwa Yule aliyeniumba – Kuniumba kutokana na maumbile salama. Maneno yake “isipokuwa Yule aliyeniumba” yanaafikiana na “… isipokuwa Allaah”. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hana mshirika katika ´ibaadah Zake kama jinsi hana mshirika katika ufalme Wake. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Zindukeni! Ni Vyake pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.” (al-A´raaf 07 : 54)

Katika Aayah hii uumbaji na amri vimewekewa kikomo kwa Allaah pekee, Mola wa walimwengu. Uumbaji wa ulimwengu na wa Kishari´ah na maamrisho ya ulimwengu na ya Kishari´ah ni Vyake pekee.

Hakika Yeye ataniongoza – Ataniongoza katika haki na kuniwafikisha kuifuata.

Na akalifanya neno – Bi maana kujitenga mbali na kila kinachoabudiwa badala ya Allaah.

Lenye kubakia katika dhuriya yake – Bi maana katika kizazi chake.

Ili wapate kurejea – Kupata njia ya kurejea kwalo, kutokamana na shirki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 73
  • Imechapishwa: 30/05/2020