2- Ufuska: Kilugha maana yake ni kutoka. Makusudio Kishari´ah ni kuacha kumtii Allaah. Kunaingia ndani yake kuacha kikamilifu. Hivyo kunaweza kusemwa kuambiwa kafiri ´fasiki`. Vilevile kuna ufuska wa sehemu. Hivyo kunaweza kusemwa kuambiwa muumini mwenye kufanya dhambi ´fasiki`. Kuna ufuska aina mbili:

Aina ya kwanza: Ufuska wenye kumtoa mtu nje ya Uislamu. Kwa msemo mwingine ukafiri. Kafiri anaitwa fasiki. Allaah alimpotaja Ibliys akasema:

فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ

“Akaasi amri ya Mola wake.”[1]

Kwa hivyo ndani ya ufuska huo kukaingia pia ukafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ

“Ama wale waliofanya ufasiki, basi makazi yao ni moto.”

Anawakusudia makafiri. Yamefahamisha juu ya hayo maneno Yake:

كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ

“Kila watakapotaka kutoka humo, watarudishwa humo na wataambiwa: “Onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mnaikadhibisha.”[2]

Muislamu anayefanya dhambi kubwa huitwa pia fasiki na ufuska wake haumtoi nje ya Uislamu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً وَلَا تَقْبَلُوا لَهُمْ شَهَادَةً أَبَدًا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Wale wanaowasingizia [machafu] wanawake watwaharifu kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi themanini na wala msipokee ushahidi wao abadani – na hao ndio mafasiki.”[3]

فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ

“Atakayekusudia kuhiji, basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala ubishi katika Hajj.”[4]

Wanachuoni walipokuwa wakifasiri ufuska hapa wamesema kuwa ni mtenda maasi[5].

[1] 18:50

[2] 32:20

[3] 24:04

[4] 02:197

[5] Kitaab-ul-Iymaan, uk. 378 cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 96-97
  • Imechapishwa: 18/03/2020