51. Nasaha za al-Khattwaab al-Makhzuumiy al-Qurashiy kwa mwanae II


1 – Usibishane sana.

2 – Usivutane na wapumbavu.

3 – Ukizungumza, basi fanya kwa ufupi. Ukifanya mizaha, fanya kidogo. Ukiketi chini, basi kaa kikao cha Tarabbu´.

4 – Tahadhari kuingiza vidole vya mkono mmoja ndani ya vengine na kuchezacheza na ndevu, pete na upanga wako. Usifukuzefukuze nzi kutoka kwako kila wakati na mengineyo yanayofanya watu kukudharau na kukusema vibaya.

5 – Kaa kwa utulivu na zungumza kwa vipengele.

6 – Msikilize yule anayekuzungumza maneno mazuri pasi na kuonyesha kupendekezwa wala kuomba yarudiwe.

7 – Yafumbie macho mambo ya vichekesho na simulizi.

8 – Usiwaeleze wengine namna unavopendezwa na mwanao, mjakazi wako, farasi wako wala upanga wako.

9 – Nakutahadharisha juu ya kuelezea ndoto zako.

10 – Usifanye mambo kama anavofanya mwanamke wala usijipinde kama mtumwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 198-199
  • Imechapishwa: 19/08/2021