51. Makatazo ya kusoma Qur-aan katika Rukuu´ na Sujuud


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kusoma Qur-aan katika Rukuu´ na Sujuud[1]. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tanabahini! Hakika nimekatazwa kusoma Qur-aan katika Rukuu´ na Sujuud. Katika Rukuu´ muadhimisheni Mola (´Azza wa Jall) na katika Sujuud ombeni du´aa kwa bidii; kwani kuna matumaini makubwa ya nyinyi kuitikiwa.”[2]

[1] Muslim na Abu ´Awaanah. Makatazo hayakufungamanishwa na hivyo yanahusu swalah zaa faradhi na za Sunnah. Kuhusu ziada ya Ibn ´Asaakir:

”Kuhusu swalah ya Sunnah, hakuna neno.” (1/299/17)

ni dhaifu na haijuzu kuitendea kazi.

[2] Muslim na Abu ´Awaanah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 117
  • Imechapishwa: 17/02/2017