51. Dalili ya waliopotea na matahadharisho ya kujifananisha nao

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya waliopotea ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

“Sema: “Je, Tukujulisheni ni wepi ambao matendo yao yamekhasirika? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia nao wakidhani kwamba wanatenda vizuri.”[1]

Kadhalika amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika mtafuata nyenendo za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge mutaingia nao.” Wakauliza: “Je, unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si wao?”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hadiyth nyingine inasema:

“Wamegawanyika mayahudi katika mapote sabini na moja, wakagawanyika manaswara katika mapote sabini na mbili na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu – yote hayo yataingia Motoni ila moja tu.” Maswahabah wakauliza: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litalokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”[3]

MAELEZO

Maneno yake:

”Dalili ya waliopotea ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

“Sema: “Je, Tukujulisheni ni wepi ambao matendo yao yamekhasirika? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia nao wakidhani kwamba wanatenda vizuri.”

Ni wale wanaomwabudu Allaah kutokana na ujinga na upotofu. Wamepotea.

Maneno yake:

Kadhalika amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika mtafuata nyenendo za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge mutaingia nao.” Wakauliza: “Je, unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si wao?”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka katika Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh).

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kupotea na kupinda kwa mayahudi na manaswara.

Maneno yake:

“Hakika mtafuata nyenendo za… ”

”Kinachodhihiri ni kwamba umaalum umetokea kwa shimo la mburukenge kutokana na kubana kwake sana na kuchukiza kwake. Licha ya hivyo kwa sababu ya kuigiliza sana nyayo zao na kufuata njia zao endapo wataingia katika mfano ufinyu kama huu na wenye kuchukiza watawafuata.”[4]

Haina maana kwamba Ummah mzima utafanya hivo. Ndani ya Ummah wako waja wema na wanaowafuata maimamu na wanazuoni. Bali makusudio ni kwamba watapatikana katika ndani ya Ummah watakaowafuata mayahudi na manaswara, watajifananisha nao na kuwaigiliza.

Tunapata faida mbili kutoka katika Hadiyth hii:

1 – Watapatikana katika Ummah huu ambao watafanya matendo ya mayahudi na manaswara.

2 – Matahadharisho kwa Ummah huu kufuata nyenendo zao wasije kupatwa na yale yaliyowapata.

[1] 18:103-104

[2] al-Bukhaariy (4356) na Muslim (2669).

[3] Ibn Maajah (3992), at-Tirmidhiy (2641) na Abu Daawuud (4596). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (171).

[4] Fath-ul-Baariy (06/498).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 21/06/2022