50. Sayyid Qutwub ndiye amesababisha Ummah kuangamia

Hii leo mimi sitambui mwanachuoni anayezingatiwa aliyewazungumzia watawala. Mnajua kuwa Shaykh Ibn Baaz aliwakufurisha baadhi ya watawala. Kuna wanachuoni waliowakufurisha baadhi ya watawala. Baadhi ya watawala wanastahiki kukufurishwa. Lakini watawala wengine bado ni waislamu. Hata kama wamepinda hakuna yeyote aliyewakufurisha. Kuna mwanachuoni yeyote anayezingatiwa kutoka katika Ahl-us-Sunnah, katika wale watu wasafi kabisa, ambaye amemkufurisha mtawala fulani hii leo? Hakuna tunaowaona wakifanya hivo isipokuwa wapumbavu, wajinga na wafuasi wa Mu´tazilah na Khawaarij. Wao ndio wenye kuwakufurisha watawala na wananchi. Wale wanaowakufurisha watawala na wanajeshi wana mwelekeo wao kutoka kwa Sayyid Qutwub. Mtu huyu ameivunja misingi ya Sunnah na akachukua misingi ya wapotevu wote. Hakuna msingi usio salama isipokuwa Sayyid Qutwub ameushika. Hakuna msingi katika Sunnah isipokuwa ameubomoa. Moja katika misingi hiyo ni kuukufurisha Ummah. Msingi mwingine ni ule ambao Takfiyr imejengwa juu yake, nao ni kwamba imani haizidi na wala haipungui. Kwa mujibu wake anaonelea kuwa imani ima iwe mia kwa mia au pia iwe ukafiri. Ima kuwepo imani au kufuru. Mtenda dhambi anayemtii mtunga sheria katika suala la upambanuzi kwa mujibu wake ni kafiri na bila ya shaka ni mwenye kutoka katika Uislamu.

Hivi kweli Khawaarij wamefikia kiwango hicho? Tunatarajia vijana watakoma na jambo hilo. Ukiweka maandiko na dalili zinazoweka wazi upotevu wa mtu huyu, hawakubali kutoka kwako. Hawataki kutafuta haki. Hawataki kushika msimamo wa kibusara kutokana na fitina hii iliyoukumba ulimwengu mzima na kuwachanganya vijana wa Ummah, imesababisha vita vya kindani na imesababisha uadui na chuki kati yao. Hawataki kuelewa, hawataki kuyasoma mambo. Hawataki kujua ni nani anayewaongoza, ni mfumo upi alionao, ni ´Aqiydah ipi alionayo na ni uelewa upi wa Uislamu alionao. Hawalitaki hilo:

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا

“Hakika mimi kila nilipowaita ili uwasamehe, huweka vidole vyao masikioni mwao na wakagubika nguo zao na wakashikilia kufanya kiburi kwelikweli.”[1]

Wamechagua mienendo hii mibaya. Mimi nasema maneno haya hata kama ndani yake mna ukali kwa sababu wapate kuamka ikiwa kweli wako na akili na wanayaheshimu maandiko ya Qur-aan na Sunnah na uelewa wa Salaf. Wanatakiwa kuyaelewa mambo haya makubwa na ya khatari ambayo yamesababisha utwevu juu ya Ummah ambao haukuwahi kutokea kabla ya Sayyid Qutwub na wafuasi wake.

Sisi tunakokoteza katika msingi huu kutokana na mitihani iliyouzunguka. Yahifadhini maandiko haya. Sisi tunamuabudu Allaah kwayo mpaka pale tutapokutana Naye. Mtu anayefuata matamanio na aliyepinda asitufanye tukapinda kutokamana na mfumo huu.

[1] 71:07

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 421-422
  • Imechapishwa: 19/11/2017