50. Maneno ya Allaah ni moja katika sifa Zake


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hiyo ni sifa ya dhati Yake, na sio kiumbe miongoni mwa viumbe Vyake.

MAELEZO

Bi maana maneno ni moja katika sifa za Allaah. Sifa zote za kimatendo pia ni sifa za kidhati. Mtunzi amesema:

“… na sio kiumbe miongoni mwa viumbe Vyake.”

Hapa wanarudiwa Jahmiyyah wanaosema kuwa Aayah inayosema:

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kikwelikweli.”[1]

maana yake ni kwamba Aliumba maneno ndani ya kiumbe. ´Aqiydah hii ni batili. Allaah alimzungumzisha Muusa maneno aliyoyasikia kutoka Kwake.

[1] 04:164

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 41
  • Imechapishwa: 29/07/2021