50. Hekima ya sita ya swawm: Kuuvunja moyo uwanyenyekee viumbe

Miongoni mwa hekima za swawm ni kuivunja nafsi na kuufanya kuwa na mpaka juu ya kiburi chake mpaka iweze kuwanyenyekea viumbe na kuwa mlaini kwa viumbe. Hakika ushibaji, kujionyesha na kuchanganyikana na wanawake ni mambo kila moja katika hayo yanapelekea katika shari, kujikweza na kuwa na kiburi juu ya viumbe na haki. Hilo ni kwa sababu pindi nafsi inapoyachagua mambo haya basi inajishughulisha kuyafikia. Inapoyaweza basi huona kuwa imefikia malengo yake. Matokeo yake inapata furaha yenye kusemwa vibaya na jeuri katika mambo ambayo inakuwa ni sababu ya kuiangamiza. Aliyekingwa ni yule ambaye amekingwa na Allaah (Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 65
  • Imechapishwa: 18/05/2020