50. Hadiyth kuhusu kusoma al-Kahf siku ya ijumaa zinapeana nguvu

Swali 50: Je, kusoma Suurah “al-Kahf” siku ya ijumaa na usiku wake ni kitendo kilichosuniwa[1]?

Jibu: Kumepokelewa juu ya hilo Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zinapeana nguvu zinazofahamisha usuniwaji wa kusoma Suurah “al-Kahf” siku ya ijumaa. Hilo limethibiti kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh). Mfano wa jambo hili halifanywi kutokana na vile anavoona mtu. Bali inajulisha kwamba yuko na Hadiyth juu ya hilo.

[1] Ahmad (1903) na Muslim (414-415).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 101
  • Imechapishwa: 07/12/2021