50. Dalili ya ishirini na tano kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

52- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah atazikunja mbingu siku ya Qiyaamah, kisha atazishika kwa mkono Wake wa kulia. Halafu atasema: “Mimi ndiye Mfalme! Halafu atazikunja ardhi saba, kisha atazishika kwa mkono Wake wa kushoto kisha atasema: “Mimi ndiye Mfalme! Wako wapi wenye jeuri? Wako wapi wenye kiburi?”[1]

[1] al-Bukhaariy (7413) na Muslim (2148).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 35
  • Imechapishwa: 11/07/2019