50. al-Fa´l na mkosi


190- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna al-´Adwaa wala at-Twiyarah. Yakweli katika hizo ni al-Fa´l.” Wakasema: “Na ni nini al-Fa´l?” Akasema: “Ni neno zuri asikialo mwanaume.”

191- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipenda al-Fa´l.

192- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Niliota usingizini kana kwamba niko kwa ´Uqbah bin Raafiy´. Tukakaribishwa tende na Ibn Twaab. Nikafasiri ndoto hiyo kama hadhi duniani, Pepo Aakhirah na kwamba Dini yetu imekomaa.”

193- Ama kuhusu mkosi Mu´aawiyah bin al-Hakam (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Kuko watu miongoni mwetu wanaoamini mkosi.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hicho ni kitu mnachohisi vifuani mwenu. Kisikuzuieni.”

Mwisho na himdi zote ni Zake Allaah.

 

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 21/03/2017