5. Matahadharisho ya mivutano


Katika misingi ya Sunnah ni:

“… kuepuka mivutano…”

Bi maana usikithirishe mijadala. Usijadili isipokuwa tu ikiwa kuna faida kama mtu ambaye una uhakika lengo lake anataka haki:

وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (16:125)

Usijadiliane na mtu mbishi ambaye lengo lake yeye anachotaka tu ni kuonesha mabavu yake na kushinda. Hii ni katika mijadala na mivutano yenye kulaumiwa katika dini. Hivyo basi, usijadili na wala usivutane. Mwenye hekima ni yule mwenye kuyaweka mambo mahala pake stahiki. Ikiwa kuna mtu mwenye kutaka umwondoshee utata, mbainishie. Toa umpe na uchukue na iwe kwa kutumia njia mazuri. Isiwe malengo yako ni kutaka kushinda. Lengo lako iwe ni kubainisha na kuweka wazi haki na kuwaongoza watu wenye kutaka uongofu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 367
  • Imechapishwa: 02/04/2017