5. Jina la mtoto linaonyesha dini yake

Nimefikiria juu ya madhambi na maasi na kuona kuwa yule mwenye kutubia basi madhambi yake yanafutwa na athari inayopelekea katika madhambi hayo. Kama jinsi Uislamu unafuta dhambi zilizotangulia (na kubwa ni shirki) basi tawbah vilevile inafuta ikiwa kumetimia masharti yake.

Hata hivyo kuna dhambi yenye kurithiwa katika kizazi. Watoto wanaipata kwa mababu zao. Hapa tawbah inahitajia mchakato mrefu. Hapa dhambi inabakiwa kuwa ni kumbukumbu tangu katika kuzaliwa kwenye vyeti vya kuzaliwa, hati ya vitambulisho, diploma, leseni, vyeti… Inahusiana ikiwa kama baba alitumia vibaya jina la mtoto kwa kutoongozwa akachagua jina linalokubaliwa na Shari´ah, lisilokuwa na lugha ya kiarabu na kuvutikiwa na maumbile yalosalimika.

Hili peke yake ni kama mto wa kifikra ambao umewakumba baadhi ya mababa kabisa. Kila mmoja anazama kwa kiasi na taathira yake ya maadili yaliyoletwa. Moja katika mifano mibaya kabisa ni kuwa baadhi yetu wana shauku iliokuwa kwa makafiri, majina mabaya yanayoangalia uzuri wa mtoto kwa kutokupenda: jina la Kishari´ah.

Namna hii ndivyo majina haya ya kigeni yamekuja kutuzuia kwa kila njia; kutoka lugha yetu, dini yetu, maadili yetu, tabiaa yetu, utukufu wetu. Wakati fulani yamepitika kwa sababu ya kughafilika, wakati mwingine ni kwa sababu ya kutokuwa na kujisalimisha. Hivyo ndio fitina hii yenye upofu ikawa imejitokeza kati ya waislamu na mapambo haya yakakosekana kwa baadhi ya watoto.

Pasina kuangalia ni nchi gani yoyote ile ya Kiislamu mtoto anazaliwa na jina lisilokuwa la kiarabu ni machungu na masikitiko. Linaudhi masikio pindi wanapolisikia na linaudhi macho pindi wanapoliona. Ikiwa anwani ya kitabu kinajuza kile kilichomo ndani basi mtu hutambua ni dini gani mtoto yuko nayo kupitia jina lake. Vipi tutaweza kuwatofautisha watoto wetu wa Kiislamu wakati kati yao kuna watoto pia wenye majina ya kikafiri?

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ni jambo lenye kushangaza kwa mtu kumnyima mtoto wake alama yake na kujififitika kwenye vijia vya kubana kwa kumpa jina lonalokataliwa na Shari´ah na linaloenda kinyume na kiarabu. Ni kana kwamba kiarabu ni lugha masikini kiasi cha kwamba hawezi kupata jina la kiarabu akampa mtoto wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 05-06
  • Imechapishwa: 18/03/2017