5 – Ahmad Shaakir kuhusu Hasan al-Bannaa na al-Ikhwaan al-Muslimuun

Shaykh Hasan al-Bannaa na ndugu zake wa Kiislamu wameifanya Da´wah hii ya Kiislamu kuwa Da´wah ya jarima na propaganda. Anafadhiliwa na wakumunisti na mayahudi. Hilo tunalijua kwa yakini[1].

Usaamah bin Ahmad Shaakir (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wakati baba yangu Shaykh Ahmad Muhammad Shaakir alipohamishwa kwenye mahakama ya Kishari´ah ya Ismaa´iyliyyah kama Qaadhiy akaniandikisha kwenye masomo ya Ismaa´iyliyyah shule ya msingi. Nilikuwa naenda kwenye darasa la tatu wakati huo. Mwalimu wa somo la kiarabu alikuwa Shaykh Hasan al-Bannaa. Alipojua kuwa mimi ni mtoto wa Shaykh Ahmad Muhammad Shaakir akaniomba kama anaweza kuja kumtembelea baba yangu. Akamkubalia. Akajadili naye juu ya kwamba Da´wah ni lazima iwe kwa Qur-aan na Sunnah. Baba akamshaji´isha kwa hilo. Mawasiliano yao yakaendelea baada ya kuhamia Cairo 1932 ambapo tulikuwa tukiishi na babu yangu Shaykh Muhammad Shaakir (Rahimahu Allaah). Pindi baba yangu alipoona kundi katika al-Ikhwaan al-Muslimuun limelemea katika vurugu akawa amekata mawasiliano yake na Shaykh Hasan al-Bannaa. Alimnasihi mara nyingi kujitenga mbali na kundi hili, lakini hakujali hilo. Mwishoni akalazimika kuandika makala “al-Iymaan Qayd-ul-Fatk” 1948-´Allaamah 1949.”[2]

[1] Taqriyr ´an Shu´uun-il-Qadhwaa´, uk. 48

[2] Min A´laam-il-´Aswr, uk. 51-52

  • Mhusika: Muhammad bin ´Iwadh bin ´Abdil-Ghaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taqriyr ´an Shu’uun-il-Qadhwaa’, uk. 48 Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 18
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadh bin ´Abdil-Ghaniy