49. Kumwomba Allaah akulinde na njia ya walioghadhibikiwa na kupotea

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ

”… si ya wale Uliowaghadhibikia… ”

Walioghadhibikiwa nao ni mayahudi waliopewa elimu pasi na kuitendea kazi. Tunamuomba Allaah atukinge na njia yao.

وَلاَ الضَّالِّينَ

”… na wala wale waliopotea!”

Waliopotea nao ni manaswara wanaomuabudu Allaah kwa ujinga na upotevu. Tunamuomba Allaah atukinge na njia zao.

MAELEZO

Maneno yake:

غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ

”… si ya wale Uliowaghadhibikia… ”

Unamwomba Allaah akulinde kutokamana na njia ya wale walioghadhibikiwa.

Maneno yake:

“Walioghadhibikiwa nao ni mayahudi waliopewa elimu pasi na kuitendea kazi. Tunamuomba Allaah atukinge na njia yao.”

Huu ni mfano uliopigwa na mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah). Licha ya kwamba mayahudi wamejua na hawakutendea kazi ndipo ikawathubutikia adhabu. Kila ambaye hakutendea kazi elimu yake basi anayo sehemu ya adhabu. Mwanazuoni ambaye ameharibika kutoka katika Ummah huu, basi ana sehemu ya ufanano na mayahudi. Mtu huyo ameghadhibikiwa.

Maneno yake:

وَلاَ الضَّالِّينَ

”… na wala wale waliopotea!”

Waliopotea nao ni manaswara wanaomuabudu Allaah kwa ujinga na upotevu.”

Huu ni mfano uliopigwa na mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah). Manaswara wanamwabudu Allaah kwa ujinga na upotofu. Kila mja ambaye ameharibika kutoka katika Ummah huu, basi ana sehemu ya ufanano na manaswara kutokana na kupotea kwake. Walioghadhibikiwa ni wale ambao wako na elimu na wasiitendee kazi. Mara nyingi hali inakuwa namna hii kwa mayahudi. Lakini wanapatikana wajinga katika wao. Amesema (Ta´ala):

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ

“Miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika; hawakijui Kitabu isipokuwa matamanio ya kudhania nao hawana isipokuwa kudhania tu.”[1]

Waliopotea ni wale wanaomwabudu Allaah kutokana na ujinga na upotofu. Mara nyingi hali inakuwa namna hii kwa manaswara. Miongoni mwao wanaweza kuwepo baadhi ya wanazuoni.

[1] 02:78

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 81-83
  • Imechapishwa: 21/06/2022