49. Du´aa kwa kitu kinachopendwa ambacho kinakhofiwa juu yake kijicho

Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ

“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Maa Shaa Allaah! Laa quwwata illa bilLLaah’ (Ametaka Allaah; hapana nguvu ila za Allaah).” (al-Kahf 18 : 39)


187- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kijicho ni haki. Lau kungelikuwa kitu ambacho kingelitangulia Qadar basi ingelikuwa ni kijicho.”

188- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu akiona kitu ambacho amekipenda kwake au katika mali yake basi akiombee baraka. Hakika kijicho ni haki.”

189- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba kinga dhidi ya majini na vijicho vya watu. Wakati kulipoteremshwa al-Falaq na an-Naas akawa badala yake anazisoma na kuacha vingine vyote.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 21/03/2017