49. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na nane wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

“Zihifadhini swalah [za kila siku] na [khaswa] swalah ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kunyenyekea.”[1]

“Zaraarah ameeleza kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Kathiyr, kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema: “Swalah ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kiongozi wa waumini, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn. Kiongozi wa waumini ndio ile swalah ya katikati:

وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

“… na simameni mbele ya Allaah hali ya kunyenyekea.”

Bi maana watiini maimamu.”[2]

Mhakiki ameelekeza hilo kwa “al-Burhaan” na “al-Bihaar”.

Hivi kweli tafsiri hii haithibitishi kuwa watu hawa ni Baatwiniyyah? Inapata kudhihiri katika tafsiri hii ya ki-Baatwiniyyah ya kwamba wanamfagilia ´Aliy juu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Uhakika wa mambo ni kuwa hawampendi si huyu na wala yule. Ni maadui wa Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maadui wa familia yake. Vovyote watakavyodai. Mwenye kusoma uhakika wa Baatwiniyyah atayaelewa haya.

[1] 02:238

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/128).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 82
  • Imechapishwa: 03/04/2017