02. Imani ni kuzungumza, kuamini na matendo ya viungo

[1] Tunaanza kwa kutaja yale ambayo Allaah (Ta´ala) ameyafaradhisha kwa waja Wake, akamtumiliza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akateremsha vitabu Vyake; nako ni kule kumwamini Allaah (´Azza wa Jall). Maana yake ni kusadikisha yale (Tabaarak wa Ta´ala) aliyosema, akayaamrisha, akayafaradhisha na akayakataza kupitia yale yote yaliyofikishwa na Mitume kutoka Kwake na yakateremshwa na vitabu. Mitume wametumwa kwa hayo. Amesema (Ta´ala):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.”[1]

[2] Imani inathibitishwa kwa kutamka kwa ulimi, kuamini na matendo ya viungo. Inazidi kwa kufanya matendo [mema] mengi na kuzungumza na inashuka kwa maasi.

Hakuna neno kwa mtu kufanya uvuaji katika imani yake. Kufanya uvuaji ni jambo halina shaka yoyote kwani ni njia iliyotumiwa na wanachuoni. Mtu akiulizwa kama ni muumini basi anatakiwa kusema:

”Mimi ni muumini Allaah akitaka.”

Vilevile anaweza kusema:

”Nataraji kuwa ni muumini.”

Pia anaweza kusema:

”Nimemwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake.”

[3] Imani na Uislamu ni maneno mawili yenye maana mbili tofauti. Uislamu kwa upande wa Shari´ah ni zile shahaadah mbili pamoja na kusadikisha ndani ya moyo ilihali imani ni ule utiifu wote.

[1] 21:25

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 20/02/2019